RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Kikwete,
amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndugu Pascal
Mabiti, kuomboleza vifo vya watu 11 ambao wamepoteza maisha yao katika
ajali ya basi iliyotokea jumatatu April 21,2014.
Aidha, katika salamu hizo raisi kikwete amesema kuwa ni jambo la
kusikitisha kuwa ajali za barabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu
wasiokuwa na hatia kila kukicha. Ameongeza, Naungana nao katika
kuomboleza wapendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu
pia. Naungana nao katika kumwomba mwenyezi mungu mwingi wa rehemz
aziweke peponi roho za marehemu.
Pia Rais Kikwete, ametoa pole kwa familia za wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment