Wednesday, August 13, 2014

MBATIA, NCHI HII HAKUNA SERIKALI

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, akiongea na wajumbe wa halimashauli kuu Taifa leo jijini Dar Es Salam.

Baadhi ya Wajumbe wa halmashaul kuu Taifa wa NCCR Mageuzi, wakiwa wamesimama ili kuwakumbuka baadhi ya viongozi wa chama hicho waliotangulia mbele ya haki.


MWENYEKITI wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia, amewataka
wajumbe wa halmashauri kuu wa chama hicho, kudumisha misingi ya amani nchini ambayo hivi sasa imepotea.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kufungua semina ya kujenga viongozi wa chama hicho, alisema kuwa amani ya nchi hii imeanza kupotea kutokana na uongozi mbaya wa chama tawala ambacho kipo madarakani.
“Tanzania ilikuwa ni kisima cha amani, lakini hivi sasa amani imetowea kulingana na ubinafsi ambao ni chanzo kikubwa cha ufisadi, sisi hatuko tayari kuona amani yetu ikipotea”alisema.

Aliongezea kuwa, sifa ya kuwa kiongozi bora ni kuonesha njia sahihi, si kukaa kimya kuona mabaya yakitokea ndipo uanze kuchukua hatua.

Aliwataka viongozi wa chama hicho, kufata na kuiga misingi ya amani ambayo baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere aliiacha, jambo ambalo litakuwa muhimili wa NCCR kwa kupata viongozi bora na wenye sifa ambayo watanzania wanahitaji.
Pia aliwapongeza wajumbe na wabunge wa chama hicho, kwa kutohudhulia kwenye vikao vya Bunge Maalmu la Katiba, kwani kwa kufanya hivyo inaonesha nidhamu ndani ya chama.

No comments:

Post a Comment