- MAHAKAMA YAKELWA NA LULU KWA KUTOFUATA UTARATIBU.
- WANASHERIA WASEMA HANA KESI YA KUJIBU.
MSANII
wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ tarehe 11/04/2012 kwenye majira ya
saa tano asubuhi alianza safari ndefu katika maisha yake ya mapambano,
safari hii akijaribu kujinasua kwenye mikono ya sheria huku ajenda kuu
ikiwa kuuonyesha ulimwengu tuhuma zinazo mkabili za mauaji ya msanii
mwenzake si za kweli.
Lulu
aliletwa mahakamani kwa siri huku akiwa chini ya uangalizi wa askari
kanzu sita kati yao wawili wakiwa wanawake wakiwa na lengo la kumficha
kwa watu pamoja na waandishi wa habari waliokuwepo mahakamani hapo
wakimsubiri baada ya taharifa kupatikana kwamba angepandishwa kizimbani.
Akisimamishwa
kizimbani mbele ya Hakimu Agustino Mmbando katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali,
Beatrice Kaganda alidai kuwa Lulu ambaye ni mkazi wa Tabata jijini Dar
es Salaam ana umri wa miaka 18.
Hatua
ambayo Lulu aliipinga vikali na kuiambia mahakama kuwa ana miaka 17.
Hapo ndipo aliposaidiwa kueleweshwa kuwa kwa utaratibu wa kimahakama
apaswi kujibu lolote katika hatua za awali na vilevile Mahakama hiyo
haina uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji, lakini yeye aliona ni bora
aanze kuweka utetezi wake vyema hata katika hatua hiyo ya awali
Kaganda
aliendelea kumsomea mashitaka yanayomkabili ambapo alidai Aprili 7,
mwaka huu eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, alimuua mtu
aliyejulikana kwa jina la Steven Kanumba. Kesi hiyo ilihailishwa na
kupangiwa kutajwa tena Aprili 23, mwaka huu mahakamani hapo.
Askari
kanzu wakisaidiwa na askari wa kawaida walimtoa Lulu mahakamani kupitia
mlango wa nyuma moja kwa moja kwenye gari aina ya Suzuki Grand Vitara
nyeupe yenye namba ya usajiri T848BNV, kwenye vioo vyake vya giza
ilisomeka PT 2565 ambayo iliondolewa kwa haraka na kusadikiwa kumpeleka
katika Gereza la Segerea.
MWELEKEO WA KESI.
Karata
ya umri hiliyo chezwa na Lulu tayari inatoa mwelekeo wa kesi yenyewe na
hivyo kumuweka marehemu -Steven Kanumba- ambaye alikuwa na umri wa
miaka 28 katika hatia kulingana na sheria ya makosa ya kijinai
yanayousiana na kujamiana. Hali hii inapunguza makali ya kesi ya mauaji
na inaweza kumfanya asiwe na kesi ya kujibu.
Kwa
umri wa miaka 17 ni mtoto na wala siyo mtu mzima hivyo kuwa na uhusiano
wa kimapenzi naye hata kama alipenda iwe hivyo unamfanya marehemu kuwa
alikuwa anakusudio au alikuwa akimbaka na hivyo kuweka kesi ya mauaji
kuwa na utetezi wa “self-defence” kwa
maneno mepesi yanampa Lulu nafasi ya kumruhusu kujitetea kuwa alifanya
lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake kujitetea dhidi ya mwanaumme mtu
mzima aliyekuwa anamkamia kumbaka.
Inaelekea
Lulu alishauliwa vema na swala la kubwatuka kwa umri alikuwa la bahati
mbaya bali lilikuwa na lengo la kumpa haki yake ya kimsingi ya
kuondolewa kwenye Gereza la watu wazima jambo ambalo mpaka sasa polisi
wetu wameendelea kulikiuka.
Faida
nyingine ya utetezi huu wa awali ni kufuta statement ambayo halihitoa
mapema kwa madai ya kuwa polisi walimlazimisha kumshikilia kwenye
korokoroni ‘Selo’ ya watu wazima na hivyo kumfanya aghafilike kiakili na
kushindwa kutoa ushahidi sahihi, kwakuzingatia hilo ataiomba mahakama
atoe ushahidi upya.
HOJA ANAZOWEZA KUJENGA KWENYE USHAHIDI MPYA
Katika
ushahidi mpya Lulu ataelezea kuwa Marehemu ndiye aliyemwita na kudai
kuwa ana mazungumzo nayeye ambayo ni muhimu yasiyo weza kungojea kesho
yausuyo tasnia ya filamu. Hivyo yeye Lulu hakuwa na kusudio la kwenda
kwa Kanumba kwa minajili ya kumwuuwa.
Ikumbukwe Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali ni
lazima athibitishe nia ya kuua ili mahakama imtie hatiani Lulu lakini
kama ni Kanumba ndiye aliyemwita mtuhumiwa nia ya Lulu kwenda kwa
marehemu kwa nia tajwa itaota mbawa.
Lulu atathibitishia mahakama ya kuwa Kanumba akuwa mpenzi wake na kwa hivyo hoja ya Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali kuwa kulikuwa na ugomvi wa mapenzi kukosa mwelekeo.
Lulu
atadai kilichomwangusha Kanumba chini na kukosa fahamu hakina uhusiano
na yeye bali ni matatizo yake ya kiafya na atatumia taarifa ya madaktari
wa Muhimbili kuthibitisha ya kuwa kilichomtoa roho marehemu ni mshtuko
mkubwa katika ubongo wake (Brain concussion) ambao
haukusababishwa na majeraha ya mwilini mwake ambayo hata hivyo hayapo.
Marehemu hakuwa na jeraha lolote kuonyesha lingeweza kumsababishia
mshtuko tajwa.
Lulu atadai mahakamani ya kuwa hakuna ushahidi wowote ule wa kitaalamu ya kuwa marehemu alikufa kwa lolote jinginelo tofauti na (Brain concussion) na inashangaza hata Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali kumfungulia
kesi ya mauaji na hivyo kumbughudhi na kumdhalilisha mbele ya jamii na
hivyo kuiomba mahakama iangalie namna ya kumfidia dhidi ya kubambikiziwa
kesi ambayo hata haipo au “malicious prosecution”.
Lulu atashanga kwanini kwenye maelezo na vielelezo vya Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali havikuonyesha
afya ya marehemu ilikuwaje kwa sababu ajuavyo yeye alikuwa akitumia
madawa mengi sana kila siku madawa yanayosadikiwa kuwa ni ya kupunguza
makali ya vvu yaani ARV na huku akiwa na tabia ya kunywa pombe kali kama
Jack Daniel, Konyagi, Whisky, Ram n.k.
Lulu
atadai ya kuwa matumizi ya madawa tajwa na vinywaji vikali kwa wakati
mmoja yalichangia katika kusitisha maisha ya marehemu na wala siyo yeye.
Pia ataikumbusha mahakama kuwa anashindwa kuelewa ni vipi daktari wa
marehemu ajashitakiwa kwa mauaji kwa kumpa marehemu madawa tajwa bila ya
vibali vya hospitali zenye mamlaka ya kufanya hivyo…………
Lakini
kubwa zaidi ni utetezi wa kimazingira ambao Lulu atautoa mahakamani
utakao onyesha kuwa yeye ni mtoto wa chini ya miaka 18 na hivyo utamweka
marehemu katika mazingira ya kiubakaji au kukusudia kumbaka na hivyo
utetezi wa self-defence kuwa na uzito wa kipekee.(kutoka media2solution.wordpress.com)
Inavyoonekana Lulu atashinda tuhuma hiyo
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletekushinda anaweza lakini yaita ji muda na atasota sana @ praygod.
ReplyDelete