Wednesday, April 11, 2012

LULU BAADA YA KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Lulu baada ya kufikishwa mahakamani kusomewa kuosa lake la mauaji ya masanii wa filamu nchini marehemu Steve Kanumba.(picha hii ni ya maktaba)
Habari hii na BBC swahlili

Msanii wa kike wa filamu nchini Tanzania Elizabeth Michael LULU, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya msanii mwingine wa Filamu marehemu Steve Kanumba.

Amefikishwa mahakamani akiwa na siku nne, tangu alipo kamatwa mara baada ya kifo cha masanii huyo amabae inaaminika kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi.


Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam Bi Agustina Mbando, Lulu aliwasili mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali chini ya Askali Polisi waliokuwa wamevaa kiraia na wengina walikuwa wamejihami kwa silaha.


Mara baada ya kufikishwa mahakamani upande wa mashitaka ukiongozw na wakili wa serikali Bi Elizabeth Kaganda ulimsomea shtaka moja ambalo ni mauaji, kosa ambalo ni kinyume na sheria kanuni ya adhabu kifungu cha 196.


Wakili huyo, alidai mbele ya mahakama kuwa mnamo 07 / 04/ 2012 , katika eneo la sinza Vatikani jijini Dar es salaam.


upande wa mashtaka umeeleza mahakama kuwa, kesi bado iko kwenye upelezi ambapo inatarajiwa kusoma tena April 23 mwaka huu mstakiwa amepelekwa  rumande hadi siku hiyo ambapo kesi itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment