Na Shomari Binda, Tarime
Siku
moja baada ya kuteuliwa kwa wakuu wa Wilaya Madiwani wa Halimashauri ya
Wilaya ya Tarime wamemkataa Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele na
kumuomba Rais Jakaya Kikwete aweze kumuondoa katika Wilaya hiyo na
kumpangia Wilaya nyingine ya kufanyia kazi baada ya kushindwa kudhititi
usalama wa Raia na mali zao na kufanya ukaidi kila anaposhauriwa.
Wakizungumza
na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhailishwa kwa kikao cha kawaida
cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kifanyike katika ukumbi wa mikutano
wa Halimashauri hiyo,Madiwani hao walidai kuwa DC Henjewele akiwa kama
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameshindwa kudhibiti matukio
ya mauajia ambapo hivi karibuni katika mgodi wa Nyamongo na Tarime Mjini
lakini Mekaa kimya.
Kiongozi
wa upinzani katika Baraza la madiwani wa Halimashauri hiyo Ndesi
Charles wa kata ya Turwa (CHADEMA) alisema wameamua kwa kauli moja
kutokufanya kikao cha Baraza la Madiwa kutokana na DC huyo kuigeuza
Halimashauri ya Tarime kama Taasisi yake na kusema kuwa hawataendesha
vikao vya Baraza hilo mpaka hapo mkuu wa Mkoa atakapokuja na kuondoka na
DC huyo.
Ndesi
amesema kuwa wameshangazwa na uteuzi uliofanyika jana wa ma DC na
Henjewele kuendelea kubakishwa katika Halimashauri hiyo licha ya taarifa
ya kulalamikiwa na Wananchi pamoja na Madiwani kwa kushindwa kuzingatia
utawala bora na kuendelea kukumbatiwa.
"Madiwani
wote tumeamua kwa pamoja kugomea kufanya kikao hicho ambacho kilikuwa
na ajenda ya kupitia taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)
lakini tumeshindwa kufanya na hatutafanya mpaka hapo DC Henjewele
atakapoondolewa katika Wilaya ya Tarime,"alisema Ndesi.
Alisema
DC Henjewele kwa sasa anafanya biashara zake na amewekeza katika mgodi
wa Nyamongo na kushindwa kufatilia kelo za Wananchi na kufikia hatua ya
kuzuia wawekezaji waliopo kuatika mgodi huo wa ABG kukataa kulipia karo
za wanafunzi kama ilivyo katika makaubaliano na mgodi huo.
Diwani
wa kata ya Nyamaraga Antony Manga (CCM) alisema suala la DC huyo
lilishaongelewa katika vikao vya chama lakini ameshindwa kuwa msikivu
katika masuala ya msingi anayolalamikiwa na Wananchi pamoja na Madiwani
hivyo nao wameamua kwa pamoja kumkataa na sio chaguo sahihi kwa Tarime
katika dhana nzima ya kuhalakisha maendeleo.
Amesema
kumekuwa na kero mbalimbali zinazomuhusu ikiwemo kutokusikiliza
kuondolewa kwa kizuizi cha Nkende kata ya Sirari ambacho kimekuwa
kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara kufanya shughuli zao za kimaendeleo
kutokana na kuwepo kwa kizuizi hicho na kudai kuwa kizuizi cha Kirumi
kinatosha.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime na Diwani wa
kata ya Sirari Amos Sagara amesema kutokufanyika kwa kikao hicho cha
kawaida cha Baraza la Madiwani ni baada ya kutokea kwa marumbano ya
madiwani wote kabvla ya kikao wakitaka kutokufanyika kwa kikao hicho
mpaka hapo atakapokuja mkuu wa Mkoa ili aweze kuondoka na DC huyo
kutokana na madai yao mbalimbali juu yake.
Alisema
baada ya maluymbano hayo kuzidi aliamua kuhitisha kikao cha ndani na
Madiwani wote na kupitisha azimio moja la kutokufanyika kwa kikao hicho
mpaka hapo watakapowasiliana na Mkuu wa Mkoa ili kushiriki katika kikao
cha pamoja na Madiwani hao ili kuweza kufikia muafaka wa yale
yanayozungumzwa.
Akiongea
kwa njia ya simu, Henjewele alisema yale yote yanayolalamikiwa na
Madiwani hao si ya kweli na kama wanataarifa za kimaandishi wanapaswa
waziwasilishe na si kuongea mambo ambayo hayana ukweli na kudai kuwa
huenda wanazo sababu zao nyingine.
No comments:
Post a Comment