Thursday, May 10, 2012

TIMU YA TAIFA YADHAMINIWA NA TBL KWA MKATABA WA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 10.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akitoa taarifa kwa vyombo vya habari amesema ni mara ya kwanza kabisa Taifa Stars kufanyiwa udhamini wa aina yake kwa mtindo mpya na wa kipekee na kuwataka Watanzania wajivunie timu yao. Ameongeza kuwa kampuni yake inakusudia kufanya kila liwezekanalo kuisaidia TFF kuhakikisha kuwa timu ya Taifa inang’ara katika anga za Kimataifa na hivyo kukidhi kiu ya Watanzania.

Mkurugenzi Mtandaji wa TBL, Bw. Robin Goetzsche ameweka wazi kuwa kampuni ya TBL itasaini Mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 10 sawa na Tsh.23 Bilioni na katika kipindi chote hicho kauli mbiu itakuwa “FIKISHA SOKA YA TANZANIA KATIKA KILELE CHA MAFANIKIO” nakuwataka Watanzania kilicho chao.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Bw. Leordar Tenga amesisitiza kuwa udhamini uliofanywa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) utaleta mapinduzi chanya katika soka nchini Tanzania na kuwaasa Watanzania kuwa hakutakuwa na haja ya kuzishabikia timu za nje badala ya kuishabikia timu ya Taifa ya Nyumbani kwa kuwa wachezaji wetu wanahitaji moyo wawapo uwanjani.

No comments:

Post a Comment