Tuesday, August 12, 2014

MTIKILA ATAKA BUNGE LA KATIBA KUSHITISHWA

Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikil.
Joto la kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba (BMK), linazidi kupanda nchini baada ya wabunge na vyama vya siasa kuendelea kusisitiza kuwa Bunge hilo halina tija kwa taifa.

Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amesema ameanza kukusanya saini za Watanzania wanaopinga kuendelea kwa Bunge hilo ili kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania, kusitisha vikao vinavyoendelea mjini Dodoma.
Mchungaji Mtikila akizungumza na Mwananchi Jumapili alisema mchakato wa kukusanya saini hizo unaendelea katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Geita, Kagera, Dar es Salaam huku akibainisha kwamba mwitio wa watu ni mzuri.
“Natafuta saini 20,000 za Watanzania na sasa tayari tumekusanya saini zaidi ya 10,000 katika mikoa kadhaa na natarajia Watanzania wataendelea kuniunga mkono ili kuhakikisha mchakato huu. Nakwenda kuuzuia Mahakama Kuu na ninajua tu nitashinda,” alisema Mchungaji Mtikila.

No comments:

Post a Comment