Wednesday, July 30, 2014
Wagombea urais Tucta waonywa
WAJUMBE wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), wametakiwa kujitambua na kujitathmini pindi wanapotaka kugombea nafasi mbalimbali katika shirikisho hilo hususani urais.
Rai hiyo ilitolewa na Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu) Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa ambaye pia katibu wa Tucta Dodoma, alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima kuhusu maandalizi na mwenendo wa mkutano mkuu na uchaguzi wa Tucta utakofanyika hivi karibuni.
Mwendwa alisema kuwa kwa sasa kuna utitiri wa watu ambao wamejitokeza kugombea nafasi ya urais wa Tucta kwa lengo la kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Rais, Juma Ayubu ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment