Thursday, July 17, 2014

KOCHA WA SERENGETI BOYS ATAMBA KUITWANGA AFRIKA KUSINI CHAMAZI

Kikosi cha Serengeti Boys

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari amesema morali ya wachezaji wake ipo juu kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) itakayochezwa kesho (Julai 18 mwaka huu). 

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. 

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo, Kocha Hababuu amesema nia ya kikosi chake ni kuhakikisha wanafika kwenye fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Niger.

No comments:

Post a Comment