Na Karoli
Vinsent
KATIBU mkuu
wa Chama cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman Kinana Ametajwa kuwa ni
mtu anayekwamisha kupatikana kwa muafaka kati ya Wajumbe wanaounda Umoja wa
Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA na Chama cha Mapinduzi CCM,baada ya kupanga
mpango wa kuwazuia Wajumbe wa UKAWA,kutoonana na Rais Jakaya Kikwete ili kupata
Suluhu,Mtandao huu umedokezwa.
Mpango huo wa Kinana unakuja baada ya kikao
cha siri kati Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini,Francis Mtungi na wajumbe wa
UKAWA pamoja na wajumbe wa chama cha Mapinduzi kikao hicho kuvunjika na
kutopatikana kwa mwafaka.
Chama
CCM ambacho ni wapangaji katika ikulu,kimeamua kupanga mpango huo
wa UKAWA kutokutana na Rais Kikwete huku wakipinga kasi waliyokuwa nao,ambayo
inaweza kubadilisha mwelekeo wa CCM,Chanzo hicho
kinasema Hofu ya Kinana pamoja na chama chake inatokana na Wajumbe wanounda
umoja huo wa UKAWA,kuwa na nguvu na kuweza kumshawishi Rais kuweza
kuyakubali Mapendekezo ya rasimu ya katiba ambayo ni pamoja na muundo wa serikali mbili.
Kitu ambacho
kinaweza kumfanya Rais Jakaya Kikwete kukubali pendekezo hilo na kupelekea
wajumbe wanaunda ukawa kurudi Bungeni,na kukiacha chama chake kikiangaika.
Wingu,zito
bado likiwa limetanda ndani ya CCM, kuhusu ni hatua zipi
zitumike hili kuokoa mchakato huo wa Katiba mpya ,ambao unaonekana kutoweza
kupatikana kutokana,hatua iliyoko sasa ambayo baada kila upande kutopatiwa
ufumbuzi huku kukiwa na jitihada za kuokoa mchakato huo zinazofanywa na msajili
wa vyama vya Kisiasa nchini kugongwa mwamba.
Hoja ya UKAWA kutaka kujadiliana na
marais wa pande zote mbili ililenga kumpa fulsa Rais Kikwete kurejesha nyuma msimamo wake
kuhusu rasimu ya pili ya katiba, maana siku alipozindua Bunge la Katiba,
aliweka msimamo ambao ndio umekuwa ukifuatwa na wajumbe wote wenye maslahi na
CCM.
Mara kadhaa, baadhi ya watu
mashuhuri na taasisi zimesema kwamba kama Rais Kikwete asingeleta msimamo wa
chama chake bungeni, ingejadiliwa rasimu ya tume, na UKAWA wasingetoka.
Miongoni mwa watu maarufu waliokiri
kwamba rais alikosea ni pamoja na Msajili ya Vyama vya Siasa mstaafu, John
Tendwa, ambaye alikiri kwamba rais aliteleza.
Jumuiya ya Wakristo Tanzania (CCT)
ilitoa waraka wake kusisitiza hoja hiyo, kwamba kauli ya rais ndiyo ilivuruga
mchakato, na kwamba ili Bunge liendelee kwa amani inabidi wajumbe wote
wajielekeze kwenye rasimu ya pili ya katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Mara kadhaa, viongozi wa UKAWA
wametamka wazi kwamba iwapo mjadala wa Bunge hilo hautajikita katika rasimu
hiyo, hawatarejea bungeni.
Serikali imekuwa inafanya jitihada
za chini chini, na za wazi kuhakikisha wajumbe wa UKAWA wanarudi bungeni,
lakini wao wanadai kwamba hawawezi kurudi kujadili rasimu ya CCM badala ya
rasimu ya wananchi iliyowasilishwa na Jaji Warioba.
No comments:
Post a Comment