Wednesday, July 30, 2014

DK. SLAA CHADEMA HAIANA MDA MCHAFU KUFATILIA MTU ANAETAFUTA URAIS


Na Karoli Vinsent

SIKU moja kupita Baada ya Gazeti makini la Tanzania Daima kufichua hujuma mbaya ya Kisiasa anayoifanya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM)  kwa kushirikiana na  wanachama waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa usaliti kwenye chama hicho.

Wanachama hao ambao wamejiunga na Chama kipya cha kisiasa cha  Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania)  chama ambacho kinaubia na Chama cha Mapinduzi CCM kwa lengo la kukiboma Chadema.

 Naye Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dk Wilbroad Slaa,ameibuka na Kumvaa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM na kusema  Chadema hakina mda wa kupoteza na kupambana mtu mwenye Tamaa ya Urais huku akijua hana sifa kushika nafasi hiyo. 

 Kauli hiyo kali Imetolewa Mda huu na Katibu huyo Mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu kwa njia ya Simu kuhusu taarifa iliyoandikwa kwenye Gazeti hilo la kila siku kuhusu mipango hiyo michafu ya kisiasa.
              
Ambapo alisema Taarifa hizo amezisikia na kusema chadema hakina mda mchafu wa kumfikilia mtu anayetafuta nafasi ya Urais huku akijua hana sifa.

No comments:

Post a Comment