Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe
akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za
Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA (Federation of East Africa
Secondary Schools Sports Association), jana katika Uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)
Mhe. Hawa Ghasia akiwakaribisha wanamichezo kutoka Afrika Mashariki
katika mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki
yanayofanyika Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 1
septemba mwaka huu 2014.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (wakwanza
kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (kulia) wakifuatilia kwa
makini matukio yaliyokuwa yyakiendelea wakati wa uzinduzi wa mashindano
ya Michezo ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama
FEASSSA jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Maandalizi ya FEASSSA
Bi.Mwantumu Mahiza akielezea jinsi Tanzania ilivyojiandaa kufanikisha
mashindano hayo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za
Sekondari za Afrika Mashariki jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar
esSalaam.
Timu
ya Mpira wa Miguu kutoka Shule ya Sekondari Makongo Tanzania katika
picha ya pamoja kabla ya mechi na Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Uganda
wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za
Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA jana katika Uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa shule za Sekondari kutoka Tanzania ambao wanashiriki mashindano ya
Shule za Sekondari za Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano ya
uzinduzi wa mashindano hayo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule za sekondari wakiwashuhudia wenzao wanaoshiriki
mashindano ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki wakiwa wa uzinduzi
wa mashindano hayo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini – WHVUM
Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini – WHVUM
No comments:
Post a Comment