RAGE APATA AJALI YA GARI
MWENYEKITI wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage, jana
amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya agari eneo Chigongwe, nje
kidogo ya Manispaa ya Dodoma, wakati akiingia mjini humo kwa ajili ya
kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba linaloanza leo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Mtandao huu wakati likienda
mitamboni, zilisema kuwa Rage amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Dodoma, akiwa na majeraha aliyoyapata yeye na watu wengine
alioongozana nao katika gari moja.
No comments:
Post a Comment