Na John Banda, Kongwa.
Akizungumza
na mwandishi wetu katika kijiji cha Mtanana alisema kuwa anaomba msaada
huo ili umwezeshe kugharimikia gharama za kumfikisha katika Hospitali
ya Mhimbili na kufanyiwa upasuaji wa uvimbe ulioko kwenye jicho.
Sekwao
alisema kuwa uvimbe huo ambao ulinza kama kipele pembezoni mwa jicho
hilo mwaka 2013,uliazidi kuongezeka na kufikia hatua ya kuvimba na
kulifanya jicho hilo kutokuwa na uwezo wa kuona.
Alisema
pamoja na juhudi za kwenda hospitali mbalimbali ikiwemo ya Mvumi, hali
jicho hilo limezidi kuvimba na waatalam wamenishauri nikafanyiwe
upasuaji kwa hatua iliyofikia.
“Kwa
kweli ninapata maumivu makali sana hivyo ninawaomba wasamaria
wema,taasisi na mashirika kunisaidia kiasi hicho cha fedha ikibidi hata
kama kuna uwezekano wa kuweza kunitibu mimi nitakuwa tayari tu ,kwani
hivi sasa nimeuza kila kitu ikiwemo nyumba,shamba na kiwanja,kwa ajili
ya kupata fedha za kujitibu”alisema.
Bi
Sekwao hata hivyo alisema kwa wale wote watakaogunswa na kilio changu
kwa lengo la kunisaidia ninawaomba watumie namba zifuatazo za simu 0687522160, 0788107753, 0682400989
No comments:
Post a Comment