Tuesday, July 22, 2014

WATU 8 WAKIWAMO MADAKTARI WA CHUO CHA (IMTU) WASHIKIRIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPA VIUNGO VYA BINADAMU KATIKA BONDE LA MBWANI MPIJI BUNJU

Kamanda wa Kanda Maalmu ya Dar es Salaam, CP Suleimani Kova, akiongea na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa taarfa kuhusu tukio la kukutwa viongo vya binadamu iliyotokea jana maeneo ya Bweni Mpiji, Alisema kuwa mifuko ya viungo vya binadamu vilivyokutwa ni eneo la tukio ni 85, awali mifuko hiyo ilionekana chuo cha mafunzo ya Udaktari Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (International
Medical and Technological University – IMTU, na Madaktari wamekili kutumia kwa katika mafunzo kwa vitendo.


Baadhi ya waandishi wa habari walioudhulia katika mkutano huo.
  
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI  JESHI LA POLISI TANZANIA

 

PRESS RELEASE 22/07/2014  WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU MAENEO YA BONDE LA MBWENI MPIJI ENEO LA BUNJU 

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watu wanane na kuwahoji kuhusu tukio la kupatina kwa viungo vya binadamu vilivyogundulika katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji ambapo mifuko ya plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu yaligundulika. Polisi walipata taarifa 21/07/2014 jioni kutoka kwa wasamaria wema na ndipo jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP. Camilius Wambura walifika hapo majira ya saa 1.00 usiku.  
Walipofika katika tukio waligundua mifuko ipatayo 85 mieusi yenye viungo vya aina mbali mbali vya binadamu kama vile,Vichwa,Miguu,Mikono,Mioyo, mapafu,vifua na mifupa ya aina mbali mbali ya binadamu. Viungo hivyo havikuwa na uvundo au harufu ya aina yoyote na vilionekana kwamba vimekaushwa na kukakamaa. 

Katika eneo hilo pia vilikutwa vifaa vinavyotumika hospitali kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves) mifuko miwili iliyotumika ,nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili zenye maswali ya kujibu. Wananchi wasiopungua 1,000 walifika katika eneo hilo la tukio lakini hakuna aliyekuwa na taarifa sahihi. Viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Aidha jopo la Wapelelezi chini ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ACP. Japhari Mohamed walianza uchunguzi mara moja kwa kusaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na uchunguzi wa miili ya binadamu (Forensic Doctor) ambaye kwa pamoja walishirikiana na madaktari wengine kutoka hospitali wa Taifa Muhimbili. Hatimaye uchunguzi wa kina ulibaini kwamba viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa katika Maabara ya Chuo Kikuu Madaktari IMTU jijinD’Salaam.
Baada ya kugundulika hivyo Polisi

wamewakamata na sasa wanaendelea kuwahoji watu wanane ambao wanasadikiwa kuhusika na miili hiyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya madaktari wa IMTU. IMTU (International Medical and Technolegical University) ni chuo Kikuu cha Madaktari ambacho pia hufanya mafunzo ya udakitari kwa vitendo (practical). Jeshi la Polisi Kanda Maalum litamuhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na hatimaye mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zake ili sheria ichukue mkondo wake. 

S. H. KOVA KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment