![]() |
Rais Barrack Obama amesema kuwa ushahidi unaonyesha kwamba
ndege ya Malaysia Airline iliokuwa ikisafiri kutoka Amstaderm kuelekea
Kuala Lumpur ilitunguliwa na kombora lililorushwa kutoka eneo
linalodhibitiwa na waasi wanaounga mkono Urusi.
Rais Obama amesema kuwa kitendo hicho kinatia hasira na
kwamba waasi hao wamekuwa wakipokea usaidizi kutoka kwa Urusi ikiwemo
makombora ya kuangusha ndege.
Obama ametaka usitishwaji wa vita nchini Ukraine ili kutoa fursa ya shirika huru la kimataifa kuchunguza kilichojiri.
Source BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment