Na Karoli
Vinsent
KATIKA
kujali ubora wa Gazeti la Mwanahalisi mtandao huu,unakuleta simulizi kuhusu
sakata la kufungiwa Gazeti hilo,ambapo gazeti hilo limefungiwa kwa mda
usiojulikana na Serikali kutokana na Habari zake zilizokuwa zikiandikwa.
Gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa Tarehe 30/07/2012 na Waziri wa Habari ,Vijana Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ambapo alitoa Hukumu ya kulifungia kwa muda
usiojulikana kwa kile alichokiita kwamba mwenendo wa Gazeti hilo si mzuri,kwani
limekuwa likiandika Makala zenye uchochezi na kuleta Uhasama na uzushi na kupelekea wananchi kukosa Imani
na Vyombo vya Dola hali inayoweza kuhatalisha Amani ya nchi.
Ambapo, Waziri huyo alitumia Sheria Kandamizi ya Magazeti ya Mwaka 1976,kifungu
Namba,25 ambayo inampa Mamlaka waziri anae husika na masuala ya Habari,
kulifungia Gazeti lolote pale yeye mwenyewe anaona kwa mawazo yake kwamba Gazeti
linakiuka sheria ya nchi.
Adhabu hiyo ilianza kutumika kwanzia Tarehe 30 mwezi Julai mwaka
2012,ambapo katika adhabu hiyo ilisema kwanzia sasa gazeti hilo limefungiwa kwa
mda usiojulikana.
Kwa sasa Gazeti hilo limetimiza Miaka miwili tangu lifungiwe lakini bado
hakuna nia ya dhati kutoka kwa Serikali katika kulegeza Adhabu hiyo kubwa
kwenye historia ya Magazeti nchini, huku serikali ikijua kwamba Nchi yetu
Tanzania iko kwenye ,Mfumo wa Kidemokrasia ambao unatoa mwanya kwa Mtu
kujieleza,
Vilevile Serikali imeshindwa hata kutambua kwamba ndani ya Katiba ya nchi
Ibara ya 18 ambayo inatoa uhuru wa
kujieleza kwa kila mtu.
Mtandao huu utakuletea Mikingano ambayo imeibuka baada ya Gazeti hilo
kufungiwa kutoka Kwa Viongozi,ambapo malamala kwa mala wamekuwa wakitofautiana
kuhusu kufungiwa gazeti hilo ambalo lilibeba Taswira ya ukombozi katika fani
hii ya Habari.
Gazeti la Mwanahalisi lilianzishwa
miaka mitano iliyopita na kuwa chini ya Kampuni ya Halihalisi Publishers
Ltd,ambapo mkurugenzi wa Kampuni hiyo alikuwa ni Saed Kubenea.
Vilevile Kubenea ambaye ni miongoni mwa Waandishi bora wanofanya Habari
za uchunguzi nchini,ambaye alikuwa anafuata nyayo za Mwandishi wa Zamani Gazeti
la Mfanyakazi Stani Katabalo,ambaye naye alikuwa ni Miongoni mwa Waandishi
wanaofanya na Kuandika Habari za Uchunguzi nchini katika kipindi hiko cha
nyuma.
Licha ya Kubenea kuwa Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo ya Halihalisi pia alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo la
Mwanahalisi.
Katika Kazi za Hatari za kufanya Habari za Uchunguzi Saed Kubenea aliwai
kukumbana na Matatizo ikiwemo kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana na
kupelekea kwenda kutibiwa nje ya nchi ili kuweza kuoka Macho yake ambayo
yalidhulika kwa Tindi kali hiyo aliyokuwa amemwagiwa Usoni hususani kwenye
Macho.
Lakini mpaka sasa Jeshi la Polisi alijawai kuwataja wala kuwakamata watu
waliohusika na kumfanyia Vitendo hivyo vya kinyama mwandishi huyo nguli katika
fani ya Habari nchini.
Gazeti hilo ambalo lilikuwa lilikuwa likifichua mambo ya mabaya
yaliyokuwa yakifanywa na Serikali,wanasiasa pamoja Viongozi wa Mashirika
mbalimbali hapa nchini.
Hii ni sehemu ya kwanza ya Sakata la kufungiwa Gazeti hili la
mwanahalisi,usikose tena kesho kujua mengine kuhusu gazeti hilo,ambapo Mtandao
huu utakuletea Simulizi ndefu kwanzia leo tarehe 21hadi tarehe 25 mwezi siku
ambayo ndio tarehe ya mwisho kuchapisha Gazeti,Nia yetu ni tunataka umma ujue na kufahamu ukweli ulioko kwenye
Sakata la Gazeti hili na Sababu iliyopeleka kufungiwa Gazeti hili.
No comments:
Post a Comment