Saturday, July 19, 2014

BODI YA MIKOPO HOI.

Picha toka makitaba.


WANAFUNZI wa elimu ya juu nchini, waitupia lawama Bodi ya Mikopo kwa kuwacheleweshea fedha za kujikimu wakati wa Mafunzo kwa Vitendo (field). 

 Wakinzungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, walisema kuwa sasa ni wiki ya Tatu toka mafunzo hayo yaanzanze lakini Bodi inatoa majibu yasiyo ya kuridhisha kwa wanafunzi hao.
Waziri wa Mikopo wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Philipo Mwakibinga, alisema kuwa wanafunzi wanaosomea ualimu bado hawajapewa hizo.

“Ni zaidi ya wanafuzi 3800 ambao hawajapata fedha hizo lakini juzi wametuma cheki ya watu 400 tu , sasa hao wengine itakuwaje?”alihoji Mwakibinga

Mwakibinga aliongezea kuwa, hali inaweza kuwa mbaya kwa wanafunzi ambao wanafanyia mafunzo hayo Mikoani kwani wanaweza kujiingiza kwenye vitendo vibaya kwaajili ya kupata fedha.

Waziri wa Mikopo wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Charles William, yeye alisema kuwa wanafunzi waliopata fedha hizo ni ni Idara (collage) 5 kati ya idara 10 zinazotolewa chuoni hapo.

Aliongezea kuwa, idara zilizopewa fedha hizo ndizo zenye wanafunzi wachache kulikuko  idara zote, hivyo ni asilimia 10% kati ya 100% waliopata fedha hizo.

“Kwakweli hali ni mbaya maana collage walizopewa pesa ni Conas, Coet, Coict, Cohu na Coss, zilizobaki ndizo zenye wanafunzi wengi ukizingatia mafunzo yalianza toka tarehe 8 kwa baadhi ya idara na wengine 15” alisema William.

William aliongezea kuwa, alijaribu kufatilia Bodi ya Mikopo, lakini alijibiwa kuwa hawajaingiziwa fedha hizo toka Benki Kuu.
Kwa upande wa Waziri wa Mikopo wa Chuo Tumaini TEKU, Hussen Ramadhani yeye alisema kuwa sasa ni wiki moja toka mafunzo hayo yaanze lakini hakuna Mwanafunzi hata mmoja aliyepata fedha.

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akijibu madai ya wanafunzi hao kwa njia ya simu yeye alisema kwa sasa hawezi kuongelea jambo hilo.

“Naomba unielewe kuwa kwa sasa siwezi kuliongelea jambo hilo kwani nikolikizo, hivyo yawezekana kukawa na mambadiliko” alisema Mwaisobwa.

No comments:

Post a Comment