BENKI ya NMB katika kuonyesha inawajali wateja wake
sasa Imezindua huduma itakayowafanya Wateja wake kufurahia Ubora wa Benki
hiyo,Baada ya Kuzindua Huduma mpya ijulikanayo “JIHUDUMIE”
Akizindua
Huduma hiyo,leo hii Jijini Dar Es Salaam, mbele ya Waandishi wa Habari na
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing alisema Kampeni inayojulikana
“Jihudumie ni huduma mpya ambayo itakayowafanya Wateja Wa Benki hiyo kufurahia
ubora na Ufanisi.
“Tunakwenda
,kuwambia wateja wetu kwamba wanaweza kutoa fedha muda wowote na mahali popote,NMB
inandelea kubuni na kuongeza huduma,kwa kushirikiana na Mitandao ya simu za
Mikononi,pamoja Huduma za ATM za Benki hii,zilizotambaa Nchi Nzima”alisema
Wiessing
Vilevile
mkurugenzi huyo alizidi kusema kwa sasa mteja wa Banki hiyo ataweza kufungua
akaunti ya chap chap chini ya Dakika 10,na kuweza kulipia bili kupitia NMB
mobile kama vile Dawasco,DSTV,TRA.
Alifanunua kwa sasa mteja wa Banki NMB,ataweza
kutuma kiasi kinachofikia milioni moja kwenda kwenye NMB mobile,ambapo huduma
hii ilikuwa tofauti na mwanzo,na vilevile kwa sasa mteja wa Banki ya NMB
anaweza kupata Huduma za Kibenki kupitia Internet
No comments:
Post a Comment