UFUNDISHAJI wa somo la ukimwi katika shule za msingi umekuwa mgumu kwa baadhi ya walimu wa masomo ya sayansi katika Kata ya Lalago, wilayani Maswa, Simiyu kwa madai ya ukosefu wa zana za kufundishia.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mbele ya wajumbe wa makundi mbalimbali ya kijamii yanayopambana na ukimwi, Hemed Burhan alisema licha ya kuwepo kwa somo hilo katika mtaala wa shule za msingi, lakini wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kutopata mafunzo zaidi licha ya kuwa wao ni walimu wa masomo ya sayansi.
Burhan ambaye pia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lalago Ufundi, alisema walimu wa kiume wamekuwa na wakati mgumu kufundisha mada ya uvaaji wa mpira wa kike (kondomu) kwa vitendo mbele ya wanafunzi wao wa kike na kutaka wapewe mafunzo maalumu juu ya kuwasilisha mada hiyo.
Alisema walimu wengi licha ya kuwa ni wa sayansi, lakini wamekuwa wakikataa kufundisha pale wanapofikia hatua kama hizo.
Akizungumzia suala hilo, Mratibu Elimu Kata ya Lalago, Ndalo Kipondya, alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa walimu wa shule tisa za kata yake ambazo zina walimu 15 wa masomo ya sayansi na asilimia kubwa ni wanaume.
Walimu hao wameiomba serikali kupitia wizara yenye dhamana kuwapatia mafunzo maalumu juu ya ufundishaji wa somo hilo na kuwapatia vifaa vya kufundishia.
Nao wajumbe wa makundi ya kijamii yanayopambana na ukimwi, wameiomba serikali kuweka msisitizo juu ya ufundishwaji wa somo hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi kuanzia darasa la nne hadi sekodari.

CHANZO TANZANIA DAIMA..
No comments:
Post a Comment