Monday, August 4, 2014

MAPYA YAIBUKA KUHUSU ASKARI FEKI

Roeson Seif Mwakyusa akishikiliwa na kachelo wa Jeshi la polisi mara baada ya kukamatwa jana huko chamanzi jijini Dar es Salaam.
Jeshi la polisi kanda maalmu ya Dar es Salaam, linamshilia na kumuhoji  Seif Mwakyusa Eemanuel miaka 30 mkazi wa kijitonyama, kwa tuhuma za kuendelea kujifanya  yeye ni afisa wa usalama balabalani.

Habari za uhakika kutoka jeshi la polisi, inasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa kweli ni askari wa jeshi la pilisi ila alifukuzwa kazi feb mwaka huu, kutokana kukiuka sheria ya jeshi hilo.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na gari no T723 BAK T/Cresta rangi nyeupe ambayo ilitumika kufanyiua utapeli, pia alikamatwa na radio Call 1,leseni za udreva zipatazo 20, sale za polisi pamoja na Ratiba ya mabasi iyendayo mikoani.

No comments:

Post a Comment