HIKI NDICHO KILICHOJILI LEO KWENYE KESI YA MBASHA
Mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel
Mbasha leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya
Ilala kujibu mashtaka mawili yanayo mkabili ya ubakaji.
Katika kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika
kuhairisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha
kwamba ana wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na
matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa
na nia ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani ilionekana
tangu kesi hiyo ianze Mbasha hakuwai kusimamiwa na wakili.
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi
wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini
mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa
alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili
tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora
Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora
ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka hu
No comments:
Post a Comment