Wednesday, August 13, 2014

TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuniUongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao tunautambua, na tutaendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu.

No comments:

Post a Comment