![]() |
Waziri wan chi Ofisi ya Waziri mkuu Willium Lukuvi (picha kutoka maktaba) |
TAASISI za kiislam Tanzania, zimepokea kwa masikitiko kauli
za kichochezi zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa juu serikalini.
“Mh Lukuvi alitamuka wazi kwamba serikali tatu zikipita eti
nchi nchi itakosa Amani! Alikwenda mbali na kutamka kuwa wanaotaka nchi yao ni
WAZANZIBARI hawawezi kujitegemea bali wanataka serikali ili wapate nafasi ya
kujitangaza kuwa nchi ya kiislamu,”alisema.
Aliongezea kuwa, kauli hizo za kichochezi zinathibidisha
kile ambacho waislam wanakilalamikia kwa mda mrefu sasa, juu ya kuwepo kwa
mfumo wa kristo unaotawala nyuma ya pazia.
Rajabu alisema kuwa, kwa miaka zaidi ya 40 sasa waislamu
wanalalamikia juu ya kuwepo na mfumo wa Kikristo unaojali maslahi ya dini moja,
ubaguzi huu ambao wamenza kuonesha utapeleka nchi hii sehemu mbaya.
Alihoji kuwa, je kauli kama hizi zinatolewa na viongozi wa
serikali, mwislamu kushutumu ukristo ndani ya msikiti hali ingekuwaje kwa
kiongozi huyo?
Hatahivyo alisema kuwa, hadi hivi sasa hakuna hatua zozote
za maana zilizochukuliwa na mamlaka husika dhidi ya kiongozi huyo kwa kauli
zake za Kibaguzi, mchozi na mwenye chuki
za wazi dhidi ya watanzania wapenda Amani na waislamu kwa ujumla.
Taasisi hiyo, imeadhimia kuwa Mh Lukuvi ajiuzuru au Rais
amwajibishe, serikali ikanushe kwa uwazi na kuomba radhi kwa waislamu na
watanzania kwa ujumla, rasimu ya katiba iliyowasilishwa katika bunge la katiba
iheshimiwe kwa mujibu wa sharia ya mabadiliko, maoni ya makundi mbalimbali
yaheshimiwe.
Pia aliwataka Waislamu na wakristo na wananchi wote kwa
ujumla kuendeleza mshikamano wao katika kutengeneza katiba mpya yenye maridhiano
yatakayoondoa kero za watanzania.
kwa mwendo huu tutafika kweli?
ReplyDelete